FreshWater Watch ni mradi wa kisayansi wa raia unaoendeshwa na Earthwatch Europe. Earthwatch ni shirika la hisani la kimazingira ambalo linazingatia sayansi, kwa lengo la kuibua mabadiliko yanayohitajika ili tuishi kulingana na uwezo wetu na kwa kuujali ulimwengu.
Kupitia kwa FreshWater Watch, tunalenga:
FreshWater Watch ilianzishwa mnamo 2012. Tangu wakati huo, shirika la Earthwatch limepanua mradi huu muhimu kuwafikia watu wanaojitoa, mashirika ya utafiti, biashara, mamlaka na shule mbalimbali kote ulimwenguni.
Kama watalamu wa maji, tunajua kwamba njia ya kipekee ya kuimarisha mazingira ni kwa kushirikiana. Ndio maana tunawaleta pamoja raia, biashara, serikali, wanasayansi na walimu mbalimbali ili kuyalinda maji safi. Kwa kusimamia mikusanyo ya maji katika mahali maalum, raia walio wanasayansi wetu kote ulimwenguni huchangia data na ufahamu kwa jitihada moja ya kimataifa ya kuimarisha uzima wa maji safi kwa kila mtu.
Makundi ya watu wanaojitoa
Huwa tunafanya kazi na makundi ya watu wanaojitoa ambayo yangependa kutumia mradi wa FreshWater Watch ili kuleta mabadiliko kwenye mazingira ya mahali wanakoishi. Kupitia kwa mradi wa FreshWater Watch, jumuia hupima na kutathmini mikusanyo ya maji wanakoishi, kukuza utambuzi kuhusu uzima wa maji safi na kuangazia uchafuzi wa madini kutokana na ukulima, viwanda na maeneo ya kushughulikia taka.
Biashara
Tunatoa fursa za kipekee ya kuwahusisha wafanyakazi na jumuia kwa washiriki wetu wa kibiashara pamoja na fursa ya kusaidia utafiti muhimu wa kisayansi. Kila mara tunasaka washiriki wapya na tungefurahi kufanya kazi nawe kuandaa mradi maalum wa FreshWater Watch ambao utatimiza mahitaji yako.
Wanasayansi
Kupitia kwa utafiti wetu, tunatumia raia wanasayansi kuangazia masuala ya kimazingira kote ulimwenguni. Tunathamini ushirikiano na washiriki wa kiakademia na taasisi za utafiti, na hivyo kutuwezesha kusambaza utaalamu wa raia wanasayansi na kutoa tafiti bora zaidi kuhusu maji safi. Mradi wa FreshWater Watch una mtandao wa taasisi za utafiti ambazo zinatalii masuala mahususi kuhusu maji safi. Taasisi zinaweza kuibuka na miradi yao maalum au kujiunga na miradi ya utafiti ya kimataifa.
Sekta ya Maji
Sekta ya maji kwa muda mrefu imetambua manufaa ya sayansi ya raia kama mbinu faafu ya kuhusisha jumuia n kuelewa masuala ya maeneo maalum, na kama nyenzo ya kutathmini uzima wa mifumo ya ikolojia na kuwezesha kuchukuliwa kwa hatua mahususi za kufanya marekebisho. FreshWater Watch ni mradi faafu kabisa kwa kampuni za maji: unatoa mbinu rahisi na inayofurahisha ya kuwezesha jumuia kutangamana na mikusanyo ya maji pamoja na kampuni za maji wanakoishi.
Shule
Earthwatch imekuwa ikifanya kazi na shule mbalimbali tangu 2016, kwa kuwahusisha watoto katika sayansi, mazingira na utunzaji. Washiriki katika vikundi maalum vya ufundishaji ni wataalamu katika kutoa mafunzo yanayojikita kwenye sayansi kwa watoto na hata walimu. FreshWater Watch ni rasilimali bora ya kielimu ambayo tunaiambatisha ndani ya programu zetu za mafunzo kama burudani, shughuli ya kufanya mwenyewe ili kuimarisha mafunzo kuhusu maji safi.
Matukio ya WaterBlitz
WaterBlitz inarejelea watu wengi kushiriki katika shughuli ya FreshWater Watch. Aghalabu hufanyika wikendi, umma unaweza kujisajili ili kupokea bila malipo kikasha cha kupima maji na hivyo kuwa wanasayansi kwa kupima maji katika eneo wanakoishi. Data inayokusanywa na mamia ya watu kupitia shughuli hizi hutupatia taswira sahihi na inayoweza kulinganishwa kuhusu ubora wa maji katika eneo fulani. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, tumeendesha WaterBlitzes Uingereza, Uswidi, Italia, Ufaransa, Ireland na Luxembourg.
Ili kuomba taarifa zaidi kuhusu jinsi tunavyofanya kazi na mashirika na taasisi kote ulimwenguni, au iwapo ungependa kushirikiana na Earthwatch katika mradi wa FreshWater Watch, tafadhali wasiliana nasi.