Jinsi ya kuongoza

Yafuatayo ni maelekezo ya hatua kwa hatua kuhusu progamu ya Sayansi ya Mwananchi juu ya mazingira ya majibaridi.
 

Nifanye nini?

  • Kifurushi cha FreshWaterWatch

  • Chombo cha kuchukulia maji, mfano chupa ya plastiki ambacho unaweza kuchukua nyumbani

  • Simu ya mpapaso yenye aplikesheni ya FreshWater Watch au karatasi ya kurekodia takwimu uyoweza kupakua kutoka kwenye ukurasa wako mtandaoni

  • Kamera kama hauna simu mpapaso

  • Penseli na saa au kifaa chochote cha kuangalizia muda.

Kifurushi chako cha FreshWaterWatch kitajumuisha maelekezo ya jinsi ya kufanya shughuli za utafafiti. Tafadhali fuatilia jinsi ya kufanya tafiti kwenye video ya mafundisho kama kuna kitu hujakielewa vizuri.
 

Muhimu: Hakikisha kuwa kila mara unaenda na mtu mwingine wa kukusaidia kufanya utafiti na pia una kibali cha kufanya utafiti kwenye maji husika aidha kutoka kwa mmiliki au meneja wa eneo husika.
 

Wapi nikafanye uchunguzi?

Unaweza kufanya FreshWater Watch katika maeneo yaliyo karibu na nyumbani, kazini au sehemu yoyote ambayo ni rahisi kwako kufika. Unaweza kufanya Uchunguzi kwenye eneo moja au maeneo mengi.

Tunahitaji kupata taarifa kutoka maeneo mengi ya maji; unaweza kutafiti mikondo ya maji, mito midogomidogo, mabwawa, maziwa, madimbwi, mifereji na maeneo oevu. Epuka kuchagua maeneo ya maji ambayo tayari yanafanyiwa uchunguzi na mamlaka za serikali.

Jaribu kuchagua maeneo ambayo yamezungukwa na mazingira mbalimbali (mfano; makazi ya watu au eneo la viwanda) au maeneo mbalimbali ya maji (mfano; mkondo wa maji au bwawa) ili uweze kujifunza mazingira ya maji ambayo yanavutia na rahisi kwako kuchunguza.
 

Lini ninaweza kufanya FreshWater Watch?

Ki msingi utafanya FreshWater Watch walau mara nne kwa mwaka: ndo kusema utatembelea maeneo yako ya kufanyia uchunguzi takribani mara moja kila miezi mitatu. Baadhi ya maeneo ya maji yanaweza kubadilika badilika kulingana na majira. Kuwa huru kufanya utafiti mara kwa mara hata zaidi ya mara nne kwa mwaka kadri uwezavyo.